Mbunge wa Viti Maalum Aysharose Mattembe Akigawa Mitungi ya Gesi kwa Wanawake Mkoani Singida.

Wanawake Mkoani Singida Wameiomba Serikali Kuweka Ruzuku katika Nishati Mbadala ya Gesi ya Kupikia Majumbani Ili kuwawezesha Watu Wengi Kununua na Kutumia Nishati hiyo Badala ya Kutumia Mkaa na Kuni Ambazo Zinawasababishia Athari za Kiafya na Kuharibu Mazingira.

Wakizungumza Mara Baada ya Kupata Mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira na Uwekezaji ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Social Mjini Singida Wanawake  hao Wamesema Semina hiyo itawasaidia Kubadili Mtazamo kwa Jamii Juu ya Ukataji wa Miti kwa ajili ya Kuni na Mkaa.

Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Aysharose Mattembe Kupitia Taasisi yake ya Mattembe Golden Women Foundation Pamoja na Mambo mengine yamewanufaisha Wanawake Kutoka Wilaya Mbalimbali za Mkoa Huo Nishati Mbadala ya Gesi ya Kupikia ili Kuepusha Matumizi ya Kuni na Mkaa.

Akizungumza Kando ya Mafunzo Hayo Mbunge wa Viti Maalum Aysharose Mattembe Amesema Lengo la Kuandaa Semina Hiyo ni Kumuunga Mkono Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Mkakati wa Utunzaji Mazingira huku Akidokeza kuwa ataendelea Kuyafikia Makundi Mbalimbali ili Kupata Ufanisi katika Utunzaji wa Mazingira.

Mgeni Rasmi katika Ufunguzi wa Semina Hiyo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida Martha Kayaga Amesema Wanawake Wengi Wamekuwa Wakipata Maradhi Kupitia Sumu Inayotokana na Moshi wa Kuni Wakati wa Kupika Huku Akiwahimiza Wanawake kubadilika na Kutumia Nishati Mbadala ya Gesi.

Amesema  Matumizi ya Nishati Mbadala ya Gesi yanarahisisha Mapishi Majumbani  na Kuokoa Muda kwa ajili ya Utafutaji Mali.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Singida Akizungumza na Wanawake Mkoani Singida


Post a Comment

 
Top