Timu ya Ihefu FC ambayo imehamishia Makazi yake Mkoani Singida Imesema Imejipanga vyema kuwababua Mashujaa Fc Ambao watakutana nao Kesho kwenye Mchezo wa Ligi Kuu ambao Utachezwa katika uwanja wa Liti.

Akizungumza na Waandishi wa Habai Mkoani Humo Kocha Mkuu wa Timu ya Ihefu FC Mecky Mexime Amesema Malengo yake ni Kuiandaa Timu yake Kuwa Tishio kwa Timu zingine anazokwenda kukutana nazo kwenye Michuano ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Mchezaji wa Timu ya Ihefu FC Raphael Daud Amesema kama wachezaji wameendelea kuhamasishana Kucheza kwa Juhudi ili kupata alama tatu zitakazowasaidia kujiweka sawa kwenye Msimamo wa Ligi Kuu.

Sikiliza Maelezo zaidi katika Video hapo chini👇👇👇

Post a Comment

 
Top