Baadhi ya Wachezaji wa Ihefu FC Wakisherehekea Ushindi wao Dhidi ya Mashujaa FC

Kocha wa Timu ya Mashujaa Fc Mwana Mapigo na Mwendo Abdallah Mohamed Bares amesema Michuano ya Kombe la Shirikisho (CRDB FEDERATION CUP) Ilikuwa ni ya Ziada kwa kwani Malengo yao Makuu ni Kupambana Vilivyo Kujiweka Sawa kunako ligi Soka Tanzania Bara.

Akizungumza na Wanahabari Mkoani Singida Baada ya Timu yake Kuondoshwa kunako michuano ya Kombe la Shirikisho kwa Mikwaji ya Penati (4-3) Dhidi ya Ihefu FC Katika uwanja wa Liti Mkoani Singida Bares Amesema Timu hiyo sasa inahamishia Nguvu katika Michezo iliyosalia katika Ligi Kuu Soka Tanzania Bara.

Kocha wa Ihefu Fc Mecky Mexime wamewataka Mashabiki wa Kandanda Mkoani Singid Kuweka Kando tofauti walizonazo na Kushikamana Pamoja ili Kuisapoti Timu hiyo ili Ifanye Vizuri katika Hatua Inayofuata.

Nahodha wa Ihefu FC Joash Onyango Achieng Ametawazwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi ya leo na kuzawadiwa Kitita cha Shilingi Laki Tano kutoka wa Wadhamini wa Michauno hiyo na Amewapongeza wachezaji wenzanke kwa Kiwango Bora walichokionyesha Katika Mchezo huo.

Post a Comment

 
Top