Ni Kibu Denis Prosper Kibu Mkandaji Jiwe Kuu la Msimbazi ambalo walilikataa Mashabiki . 

Kiungo huyu mshambuliaji wa klabu ya Simba aliposajiliwa na Klabu hiyo Mwezi Agosti 2021 kwa Mkataba wa Miaka miwili akitokea Mbeya City Mashabiki waliubeza sana Uwezo wake Kiasi cha Kudiriki kusema Hana Hadhi ya Kucheza katika Klabu ya Simba ingawaje Makocha Kadhaa waliopita Msimbazi Walimwelewa sana Mvuja Jasho huyo Ama hakika Mvulia Juani Hulia Kivulini. 

Mchezaji huyu Mzaliwa wa Mwaka 1998 Muda huu yupo kwenye nafasi nzuri zaidi ya Kula Kivulini kutokana na Ofa kadhaa anazohusishwa nazo Baada ya Kiwango Bora alichokionyesha Kunako Michezo Mbalimbali akiitumikia Klabu ya Simba. 

Taarifa kutoka vyanzo Mbalimbali zinasema Mchezaji huyo ambaye Mkataba wake unakoma Mwishoni mwa Musimu huu Tayari ana Ofa ya mshahara wa Milioni12 kwa mkataba wa miaka 2 na pesa ya Usajili ambayo ni Shilingi Milioni 300 kutoka katika klabu moja hapa Nchini Tanzania. 

Taarifa Mbalimbali zinadai kwamba Viongozi wa Simba SC Wamekuwa wakimbembeleza Mchezaji huyo kwa Miezi kumi sasa ili Kuongeza Mkataba wake lakini Juhudi Bado hazijazaa Matunda. 

 Taarifa za Awali Kabisa Zilidai kwamba Kibu Denis alipata ofa ya kucheza nchini Norway ingawaje pia Zipo Tetesi za Mchezaji huyo Kuhusishwa na Klabu ya Wydad Casablanca ya Pale Morocco.

 
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top