Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili Akikabidhiwa Mwenge Kutoka kwa Mmoja wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  Abdallah Shaib Kaim Ameipongeza Hospital ya Mtakatifu Carolous Wilayani Singida kwa Kuanzisha Mradi wa Uzalishaji Maji Tiba (Drip Water) ambayo yanasaidia katika Utoaji wa Huduma za Afya Katika Baadhi ya Vituo vya Afya vya Wilaya Hiyo.

Akizungumza Mara Baada ya Mwenge wa Uhuru Kuutembelea Mradi huo Pamoja na Kukagua Program zingine za Ukimwi na Malaria zilizopo katika Hospitali hiyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Amesema Mwenge uhuru umependezwa na Hatua ya Hospitali hiyo Kuzalisha Maji hayo na Wanatambua kwa Dhati Mchango wao katika Utoaji wa Huduma za Afya kwa Wananchi wa Eneo Hilo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Shaib Kaim Akikabidhi Vyandarua kwa Akina Mama katika Hospital ya St. Carolous Baada ya Kukagua Program za Ukimwi na Malaria.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida Dr Grace Charles Ntogwisangu Amesema Mradi wa Maji Tiba Unaofanywa na Hospitali hiyo Pia Umesaidia kwa Kiasi Kikubwa katika Shughuli za Ujifunzaji kwa Wanafunzi wa Masomo ya Sayansi katika Baadhi ya Shule za Sekondari Wilayani Humo.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida Dr Grace Charles Ntogwisangu Akitoa Maelezo kwa  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Shaib Kaim Kuhusu Mradi wa Maji Tiba.

Mwenge wa Uhuru Umekimbia zaidi ya Kilomita Mia Moja Kumi na Nane Katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambapo umezindua na kuweka Mawe ya Msingi katika Miradi mbalimbali yenye Thamani ya Zaidi Milioni Mia Tano.


Post a Comment

 
Top