Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mosses Machali(Katikati) Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda(kushoto) katika Kata ya Msingi Wilayani Mkalama.

Wananchi wa Kijiji cha Malaja Wilaya Mkalama Wameishukuru Serikali ya Tanzania Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Kufanikisha Ujenzi wa Miundombinu ya Mradi wa Maji ambao unakwenda kuwaondolea Adha ya Kufuata Maji Umbali Mrefu.

Wakizungumza Baada ya Mwenge wa Uhuru Kuweka Jiwe la Msingi katika Mradi Huo Wananchi Hao Wamesema Kabla ya Mradi Huo Walizamika Kutembea Umbali kwa Zaidi ya Kilometa Sita Ili Kupata huduma ya Maji ambayo pia walikuwa Wakichota kwenye Madimbwi.

Akiwasilisha Taarifa ya Mradi huo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Meneja wa RUWASA wilayani Mkalama Mhandisi Christopher Saguda Amesema Mradi Huo Umegharimu zaidi ya Milioni Mia Tano na kwamba Unakwenda kuwa Mwarobaini wa Magonjwa yatokanayo na Ukosefu wa Maji Safi na Salama kwa Wakazi Hao.

Wafanyakazi wa RUWASA katika Picha ya PAmoja Mara Baada ya Kuwasilisha Taarifa ya Mradi wa Maji Malaja kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa.

Mbunge wa Iramba Mashariki Francis Isack Amesema Mradi wa Maji katika Kijiji cha Malaja unakwenda Kumtua Mama ndoo Kichwani Huku Akiwataka Wananchi katika Eneo Hilo Kuulinda Mradi huo kwa Wivu Mkubwa Mradi huo wa Maji.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa  Abdallah Shaib Kaim ameiagiza RUWASA Wilayani Mkalama Kumaliza kwa Wakati Mradi Huo ili Wananchi Wapate Huduma ya Maji Karibu na Makazi yao.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdallah Shaib Kaim Akizungumza na Wananchi Wilayani Mkalama Wakati wa Mbio za Mwenge Wilayani Humo.

Mwenge wa Uhuru Wilayani Mkalama Umekimbia Zaidi ya Kilometa Mia Moja Hamsini na umeweka Jiwe la Msingi katika Mradi wa Maji Malaja na kuzindua Miradi Mbalimbali Wilayani Humo Ambayo ina Thamani ya Zaidi ya Bilioni 1.7 na Mkuu wa Wilaya Hiyo Mosses Machali Amesema Miradi hiyo Inakwenda Kubadili Maisha ya Wananchi Wilayani Humo.


Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida Munira Nkango Akifurahia Jambo na Mkimbiza Mwenge katika Mapokezi ya Mwenge Huo katika Kata ya Msingi Wilayani Mkalama.



Post a Comment

 
Top