Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba Akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoani Singida.

Mkuu wa MKoa wa Singida Peter Serukamba amewahimiza Wabunge na watendaji wengine wa  Mkoa huo kushirikiana katika  kutafuta fedha za ujenzi wa miundombinu ya barabara  badala ya kutegemea bajeti ambayo imekuwa haitoshelezi kufikisha Miundombinu hiyo  maeneo yote ambayo bado yanauhitaji. 

RC Serukamba amesema hayo kwenye kikao cha 46 cha Bodi ya Barabara cha Mkoa wa Singida ambapo Wakala wa Barabara Nchini TANROADS inahitaji jumla ya shilingi Bilioni 97 ya Bajeti kwaajili ya  kutekeleza ujenzi na Ukarabati wa Mtandao wa Barabara za TANROADS wa Zaidi ya Kilomita 1700 kwa Mkoa mzima katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Katika hatua nyingine RC Serukamba amewataka viongozi wa mkoa huo kuwa na Mawasiliano na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo ile ya miundominu ya Barabara.

Baadhi ya Wajumbe ambao Wameshiriki Katika Kikao cha Bodi ya Barabara.

Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida Mhandisi Msama Msama amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya miradi 10 ya barabara  yenye jumla ya Kilomita 635.9 Itatekelezwa.

Post a Comment

 
Top