Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili Akisalimiana na Mkandarasi Mkuu wa Mradi wa REA.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Singida ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Muragili Amezindua Mradi Mpya wa Usambazaji wa Umeme wa REA Katika Vijijimiji Wenye Thamani ya Zaidi ya Shilingi Bilioni Saba Utakaotekelezwa katika Kata Tisa Zilizopo pembezoni wa Manispaa ya Singida.

Akizungumza Katika Uzinduzi wa Mradi Huo ambao umefanyika katika Kata ya Mwankoko Manispaa ya Singida Mhandisi Muragili Amesema Mradi Huo unakwenda Kuhitimisha Ukamilifu wa Umeme katika Maeneo ambayo hayakuwa na Umeme katika Manispaa ya Singida.

Mhandisi Muragili Amewaomba Wananchi Kuchangamkia Fursa za Kuunganishia Umeme huo kwa Gharama nafuu ya Shilingi 27,000 Huku akiwahimiza Kuibua Shughuli za Uchumi kupitia Umeme huo ili Kukuza Vipato vyao.

Kaimu Mkurungenzi wa Mipango na Utafiti Kutoka Wakala wa Usambazaji wa Umeme Vijijini REA Nicolaus Moshi Amesema Mradi Huo wa REA Awamu ya Tatu Utajenga Kilometa 40.5 na Unatarajiwa Kutekelezwa Katika Kipindi cha Miezi Kumi na Tano.

Baadhi ya Viongozi ambao Wameshiriki katika Uzinduzi Huo wameishukuru Serikali kwa Jitihada za Kupeleka Umeme Maeneo Mbalimbali Nchini na Kwamba Hatua Hiyo itasaidia kwa Kiasi Kikubwa Kuchochea Maendeleo Nchini.

Cc @irundetz

#irundereports

Post a Comment

 
Top