Serikali Mkoani Singida Imesema inajivunia Mafanikio Makubwa katika Sekta ya Kilimo kutokana na Uzalishaji Mkubwa wa Mazao ya Chakula yanayochagizwa na uwepo wa Zana Bora za Kilimo na Upatikanaji wa Pembejeo.

Akizungumza katika Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika Mkoani Singida Ambayo yamefanyika Kimkoa Wilayani Mkalama,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Singida Evodius Katale amesema Uzalishaji huo unatokana na Ufanisi wa Mikakati ya Mkoa Kuhamasisha Kilimo ili Kumaliza Tatizo la njaa na kuacha kutegemea Msaada wa Chakula kutoka Serikalini.

Amesema uzalishaji huo unaufanya Mkoa wa Singida kuwa na chakula cha kutosha Kutokana na Ongezeko la zaidi ya Tani Laki Sita kwa Mwaka 2021/2022 Tofauti na Mwaka 1990 ambapo Uzalishaji wa Mazao hayo Ulikuwa Takribani Tani Laki Mbili. 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Asia Messos amewakata Wananchi Wilayani humo Kutimiza Majukumu yao Pamoja na Kushiriki Vyema katika Shughuli za Maendeleo Ikiwemo Kujitolea kwenye Michango Mbalimbali Ili Kuharakisha Maendeleo ya Wilaya hiyo.

Amesema Mkalama ina Mchango Mkubwa katika Harakati za Uhuru wa Tanganyika na Kwamba Imepiga hatua Kubwa katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake kutokana na Ukusanyaji mkubwa wa Mapato unaofanya waweze Kujitegemea Licha ya Uchanga wa Wilaya Hiyo. 


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama James Mkwega amesema kipindi mkalama inategemea kila kitu kutoka Wilaya mama ya Iramba Wananchi walikuwa na changamoto katika kupata huduma Mbalimbali tofauti na sasa. 

Cc @irundetz

#irundereports



Post a Comment

 
Top