Timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa Kutinga Hatua ya 16 Bora Katika Kombe la Dunia Baada ya kuibamiza Timu ya Taifa ya Ecuador kwenye Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea Nchini Qatar.

Simba hao wa Tereranga Ambao ndio Wanabeba Matumaini ya Afrika walikuwa wa Kwanza Kuandika Bado Dakika ya 44 kupitia kwa Ismail Sarr kwa njia ya Mkwaju wa Penality kabla ya Wapinzani wao Ecuador Kujitutumua na Kusawazisha Goli Hilo Dakika ya 68 kupitia kwa Moses Caicedo.

Bao Hilo Hata Hivyo Halikudumu Baada ya Kalidou Koulibaly Kupigilia Msumari wa Pili Dakika Mbili Baadaye ya Dakika ya 70.

NB: VIPI CHAMA LAKO? AU HAYATUHUSU.

Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top