Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Singida Umetoa Mahitaji kwa Wazee katika Kituo cha Sukamahela Pamoja na Kushiriki Shughuli Mbalimbali Ikwemo Kusafisha Makazi ya Wazee Hao ambayo yapo Pembezoni Mwa Zahanati ya Sukamahela Wilayani Manyoni.

Mwenyekiti wa Mtandao huo Ambaye Pia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida ACP Stella Mutabihirwa Amesema Wamechangua Kulisaidia Kundi Hilo Kwa Sababu Limeonekana Kutengwa na Jamii huku Akiwahimiza Watu Kujitokeza Kuwasaidia Wazee hao Mahitaji Mbalimbali.

Kamanda Mutabihirwa Amewahimiza Wazee Wanao ombaomba Barabarani Kuacha Utamaduni Huo Badala yake Waende kwenye Vituo vya Kulea Wazee ili Kupatiwa Msaada kwani Serikali inawajali na Kwamba Barabarani Sio eneo Salama Kwao.

Mrakibu wa Polisi Elina Maro Amesema Mtandao wa Polisi Wanawake Mkoani Singida umeamua Kutoa Msaada huo kwa Kundi hilo kwa Sababu Lionekana Kusahaulika Kwenye Jamii.

Afisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi katika Kituo cha Kulea Wazee Wasiojiweza Sukamahela Yolanda Komba Amesema Changamoto Kubwa Wanayoipata kwa Wazee wanao ombaomba Barabarani ni Kukataa Kukubali Kulelewa Kwenye Kituo Hicho na kwamba wao Kuombaomba ni Hulka Waliojijengea.

Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top