Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba Akihutubia Wakati wa Hafla ya Kukabidhiwa Madarasa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba Amewataka Wazazi,Waalimu na Wanafunzi Mkoani Humo Kushirikiana kwa Pamoja Kutokomeza Daraja Sifuri na Daraja la nne katika Matokeo ya Kidato Cha Nne.

Akizungumza Kwenye Hafla ya Kukabidhiwa Madarasa Kimkoa ambayo imefanyika katika kata ya Issuna Wilayani Ikungi Mkuu Huyo wa Mkoa Amesema nia ya Mkakati huo inachagizwa na Jitihada za Serikali katika Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa Kinara Katika Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa Tofauti na Awamu Zilizopita huku Akiwahimiza Waalimu na Wanafunzi Kutimiza Wajibu wao ili Matokeo Chanya ya Uboreshaji wa Miundombinu hiyo yaonekane.

Aidha Mhe.Serukamba Amewapongeza Viongozi wa Wilaya ya Ikungi kwa Kukamilisha kwa Haraka Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa huku Akiwataka Viongozi wa Wilaya Zingine za Mkoa Kuiga Mfano huo ili kuharakisha Maendeleo.

Amesema Viongozi wa Wilaya pamoja na Halmashauri ya Ikungi wamekuwa Wakifanya Kazi kwa Umoja na Mshikamano Kiasi Kilichomfanya Kuwaalika Viongozi kutoka Wilaya zingine katika Halfa hiyo ili Kujionea Kazi Kubwa iliyofanyika Wilayani Ikungi.

Awali Akiwasilisha Taarifa kwa Mkuu wa Mkoa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi Amesema Halmashauri hiyo ilipokea Shilingi Milioni 580 kwa Ajili ya Ujenzi wa Madarasa 29 katika Shule 16 na Kwamba Tayari Ujenzi wa Madarasa hayo Umekalimika.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi Justice Kijazi Akiwasilisha Taarifa kwa Mkuu wa Mkoa
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro Amesema Ujenzi wa Madarasa yote 29 Umetekelezwa kwa Viwango na kwa muda uliopangwa huku Akiwahimiza Waalimu na Wanafunzi kutunza Miundombinu hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro Akizungumza katika Hafla ya Kukabidhi Madarasa.


Cc @irundetz

#irundereports

Post a Comment

 
Top