Kamati ya Siasa ya Kata ya Mandewa Manispaa ya Singida imesema Haitakuwa Tayari Kupokea Mradi wa Kituo cha Afya Mwaja kutokana na Dosari Kadhaa Zilizojitokeza na Imemuomba Rais Samia Suluhu Hassan Kutuma Timu Kuja Kukagua Mradi Huo.

Wakizungumza na #Wasafimedia Mara Baada ya Kukagua Mradi huo Wajumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Mandewa Wamesema Chama Cha Mapinduzi lazima Kisimamie Haki za Wananchi wa Mandewa Hivyo Hakitakuwa Tayari Kuupokea Mradi Mchafu ambao Serikali imetoa Mamilioni ya Fedha.

Akizungumza na #WasafiMedia Singida kwa njia ya Simu Mhandisi wa Manispaa ya Singida Mhandisi Mligo Amesema Tatizo la Baadhi ya Milango Kuachia Mianya wanalitambua Huku akibainisha kuwa Mbao hazikukauka Vizuri wa Matengenezo.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Jeshi Lupembe Amesema ni Kweli Mradi Huo una Kasoro kadhaa na Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU)Imeanza Kuuchunguza na Uchunguzi utakapokamilika Wahusika Watachukuliwa Hatua.


Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top