Timu ya Polisi Tanzania Leo inashuka Dimbani Kuminyana na Simba Sc katika Mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ambao utachezwa leo Saa Kumi Jioni Katika Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi Kilimanjaro.

Kaimu Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Juma Mgunda Amesema Timu hiyo imejiandaa Kupata Matokeo Mazuri katika Mchezo huo kwani Matokeo Hupatikana Sehemu yeyote.

Simba Sc inashuka Dimbani leo Ikiwa na Kumbukumbu ya Kutoshana na nguvu na Wagonga Nyundo wa Jiji la Mbeya,Mbeya City Huku Wenyeji wao Polisi Tanzania wao Wakiwa na Kumbukumbu ya Kichapo cha 2-1 Kutoka kwa Wakata Miwa Mtibwa Sugar.

Maafande Hao wa Polisi Tanzania Kupitia Kurasa zao za Mitandao ya Kijamii Wamejinasibu kuwatungua Simba Sc katika Mchezo Baada ya Kurejea Kuutumia Uwanja wao wa Ushirika. 

Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top