Klabu ya Simba Imefanikiwa Kuibuka na Alama Tatu Baada ya Kuibamiza Polisi Tanzania 3-1 Katika Mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ambao Umechezwa Leo Katika Dimba la ushirika Mjini Moshi Kilimanjaro.

Simba Sc Imevuna alama Hizo Muhimu Leo na kuwapa Furaha Mashabiki wao Ambao Wametoka Kuhuzunishwa na Matokeo ya 1-1 Dhidi ya Mbeya City Katika Mchezo Uliopita.

Kwa Upande wao Maafande Polisi Tanzania Wameendelea Kugugumia Maumivu ya Kupoteza Mchezo Mwingine Mara Baada ya Kupoteza Mchezo Uliopita Dhidi ya Wakata Miwa Mtibwa Sugar.

Mchezaji wa Simba Sc Moses Phiri leo Amefufua Matumaini ya Kuwania Kiatu cha Dhahabu mara Baada ya kuongeza Magoli Mawili na Kufikisha Jumla ya Magoli 8 Katika Akauti yake ya Magoli Musimu huu.

Cc @irundetz
#irundereports

Post a Comment

 
Top