Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kutunga Sheria ndogo itakayotumika kuzuia mifugo wanao randaranda mitaani na kufanya uharibifu wa miti iliyopandwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.

Maelezo hayo ameyatoa leo katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo alipokuwa akitatua kero za Wananchi waliokuwa wakilalamikia uwepo wa mbuzi wanaozurura mitaani na kuharibu miti na mazao mengine yaliyopandwa.

Akitolea ufafanuzi swala hilo Mkuu huyowa Mkoa  amemuagiza aliyekuwa akikaimu nafafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Huseni Sepoko kuhakikisha kwamba katika kipindi kifupi wawe wametunga Sheria ndogo ambazo zitawasaidia kuzuia wanyama wanaorandaranda ambayo itaruhusu kuwakamata mifugo hiyo na kuwapiga faini.

Mkuu wa Mkoa Peter Serukamba Akizungumza Wakati Akitatua Kero za Wananchi Wilayani Iramba.

"Nakuagiza Mkurugenzi katika kipindi kifupi kijacho mtunge Sheria ndogo ambazo zitazuia mifugo kuzurura mitaani, na mhakikishe Sheria hiyo inaweza kutoa adhabu kali kwa watakao kiuka utaratibu". RC Serukamba

Amesema kwa sasa ni mpango wa Mkoa kuhakikisha kwamba kunapandwa miti zaidi ya Milioni tatu na kuifanya Singida kuwa mji wa kijani jambo ambalo haliwezi kufanikiwa endapo miti hiyo itaendelea kuharibiwa na mbuzi wazururao.

"Mkoa tumepanga kupanda miti zaidi ya Milioni tatu, tutashirikiana na wanafunzi, Makanisa na Misikiti kuhakikisha kila kaya inakuwa na miti isiyopungua minne, hatutavumilia jitihada hizo zikwamishwe kwa uzembe" Serukamba.

Aidha amewataka viongozi wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanawafuata wananchi walipo na kutatua kero zao badala ya kukaa ofsini kusubiri viongozi wa ngazi ya juu wanapotoka na kila mtumishi ahakikishe anakamilisha majukumu yake kwa wakati.

Akiwa katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa ameweza kusikiliza jumla ya kero 32 zikiwemo za ardhi, maji na madeni na usafi wa Mazingira.


Post a Comment

 
Top