Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ikungi Juma Ally Mwanga(Kushoto) Akimpongeza Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu wa Kutunuikiwa Tuzo.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtataru Ametunukiwa Tuzo ya Heshima na Taasisi ya Tanzania Youth Elite Community Kutokana na Mchango wake katika Usimamizi na Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali Jimboni Mwake.

Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Tuzo hiyo Katibu Mkuu wa Taasisi Hiyo Ng'wigulu Nyerere Shigela Amesema lengo la Kuanzishwa kwa Tuzo hizo ni Kutambua Mchango wa Watu katika Jamii ili Kuwaongezea Ari ya Kujituma zaidi Kuisaidia Jamii.

Amesema Taasisi hiyo yenye Makao Makuu yake Arusha Tayari Imetoa Tuzo kwa Watu Mbalimbali nchini ambapo Mkoani Singida ni Watu wawili Pekee Wametunukiwa Tuzo hiyo ambao ni Miraji Mtaturu Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Kada wa CCM Suphiani Nkuwi ambaye ameshida Tuzo kutokana Mchango wake wa Kuisemea Vizuri Serikali.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu Akizungumza Mara Baada ya Kupokea Tuzo hiyo Amesema Ufanisi wake katika Kusimamia na Kutekeleza Miradi Mbalimbali Jimboni Mwake unatokana na Uongozi Makini wa Halmashauri na Wilaya ya Ikungi Pamoja na Ushiriki Mkubwa wa Wananchi Katika Shughuli Mbalimbali za Maendeleo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ina Mchango Mkubwa katika Tuzo hiyo Kutokana na Namna Inavyotoa Fedha Nyingi kwa Ajili ya Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali.

Viongozi Mbalimbali  wa Wilaya ya Ikungi ambao Wameshiriki katika Hafla ya Kukabidhiwa Tuzo hiyo Wamempongeza Mbunge huyo kwa Kupewa Tuzo hiyo Huku Wakisisitiza kuwa Amesistahili Kupewa Tuzo.

Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top