Wakandarasi waliofanikiwa kupata tenda ya Ujenzi wa barabara Mkoani Singida wametakiwa kufanya kazi kwa weledi na kukamilisha kazi kwa wakati kama walivyokubaliana katika mikataba yao ya kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba wakati wa utiaji saini baina ya Wakandarasi hao na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

Aidha Serukamba  amewataka Wakandarasi hao kuondoa kero za usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Mkoa huo kwa kuhakikisha wanajenga Barabara zenye ubora wa hali ya juu na kuzikamilisha kwa wakati ili wananchi waweze kurahisisha maisha yao.

Hata hivyo RC Serukamba amewataka TARURA kusimamia kikamilifu Wakandarasi hao kwa kuwa Serikali imetoa fedha zaidi ya Bilioni 21.2 kwa ajili ya Ujenzi wa barabara za Mijini na Vijijini na kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana.

Aidha RC Serukamba amewaagiza TARURA, TANROAD na RUWASA Mkoani hapo kuanza utaratibu wa kufanya tathmini baada ya kumaliza taratibu za kutoa tenda kwa Wakandarasi ili kupima mchakato ulivyokwenda na kuona kama kulikuwa na makosa yaliyotolewa awali.

Hata hivyo ameeleza kwamba ni lazima taarifa hizo ziwe za wazi ambapo walioshindanishwa wanaweza kuona utaratibu u"Tukimaliza manunuzi yote kwa mwaka TARURA, TANROAD na RUWASA muwe na checklist inayoonesha tenda zilizofanyika na mchakato ulivyokwenda moja kumpatia Mkandarasi, rushwa haiondolewi ki babe bali inaondolewa kwa mfumo" alisema RC

Awali akitoa taarifa yake Meneja wa TARURA Mkoa wa Singida Mhandisi Tembo David amesema TARURA katika mwaka wa fedha wamepanga kutengeneza Barabara zenye urefu wa km 944 na kujenga jumla ya madaraja na vivuko 72.

Aidha Mhandisi Tembo ameeleza kwamba TARURA Singida wamejipanga kufanya matengenezo ya kawaida ya Barabara kwa urefu wa Km 483 na matengenezo ya sehemu korofi zenye urefu wa km 224 pamoja na matengenezo ya muda maalum yenye urefu wa km 237.

Pamoja na mambo mengine TARURA itatekeleza majukumu ya utenegenezaji wa madaraja na vivuko 72 na Ujenzi wa barabara za kiwango cha lami chenye urefu wa km 5.1 na km 550 ambazo zitajengwa kwa kiwango cha changarawe na km 388.9 kiwango cha udongo.

Aidha Mhandisi Tembo amesema utekelezaji wa Ujenzi wa barabara umefikia asilimia 30.

Kwa niaba ya Wakandarasi walioweza kupata tenda hizo Siamen Kimaro Mkurugenzi wa Kampuni ya Tanlite Labour Based Contractor amesema watahakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kumalizi kwa wakati huku akiahidi ubora mkubwa katika kazi waliyopata.livyokwenda mpaka kupatikana washindi.

RC amesema utaratibu huo utasaidia kuondoa rushwa katika mchakato mzima wa kupata Wakandarasi wenye sifa na ubora na kusaidia kuona makosa yaliyofanyika awali ambayo hayataweza kurudiwa katika kipindi kingine.


Post a Comment

 
Top