Irunde Reports ni blog ama tovuti ya binafsi inayojihusisha na shughuli za kiuandishi kama kuhabarisha,kuelimisha,kuburudisha,na kuutaarifu umma wa watanzania juu ya masuala mbalimbali yenye maslahi mapana katika maisha yao ya kila siku.


Tovuti hii maridadi inamilikiwa na Bwana Fedinand Filbert Irunde ambaye pia ni Mkurugezi wa tovuti hii.

Tovuti hii ilianzishwa mnamo 25.04.2013 ikiwa inafahamika kwa jina la Mtumwire blog kabla ya kuwa Voice of bongoland.


Mkurugenzi wa Tovuti hii Bwana Irunde aliamua kubadili jina la awali la tovuti hii ili kusadifu maudhui ya tovuti hii ambayo ni kupaza sauti za umma wa watanzania ndio maana akamua kuiita Voice of bongoland yaani sauti ya Ardhi ya Tanzania ingawaje pia V.O.B news ilikuwa sio neno Rahisi sana Kwa Hadhira ndio maana Sasa Tovuti hii Inajulikana kwa jina la Irunde Reports.


Maudhui ya tovuti hii ni kuzifanya sauti za wasio na sauti ama wanyonge katika ardhi ya Tanzania kusikika kwa urahisi katika ngazi zenye dhamana ya juu serikalini ili kutoa suluhu ya kudumu juu matatizo yanayowakabili.


Tofauti na tovuti zingine Irunde Reports inalenga kutupia macho ya ukaribu kwa makundi ya watu ambao sauti zao zimesahaulika mfano,sehemu za vijijini,watu wasiojiweza kama wazee,walemavu na wengineo wengi ambao pia sauti zao bado hazisikiki.


Mfano wa Daraja ambalo kwa kawaida huunganisha pande mbili za barabara ndivyo ilivyo kwa tovuti hii ambayo kazi yake ni kuunganisha umma wa watanzania na viongozi wao katika kutoa maamuzi juu ya masuala mbalimbali yanayoihusu nchi yao.


Muungano huu mithili ya daraja unaozungumziwa katika tovuti hii pia unahusisha nia ya dhati ya kuwaleta pamoja watanzania katika kujadili na kutoa mitazamo ya yao kutokana na mada mbalimbali ndani ya tovuti hii zenye maslahi mapana kwao mfano kijamii,kiuchumi,kisiasa na kielimu kwani siku zote Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.


Irunde Reports kama Tovuti huru,inalenga kufanya kazi kwa mapana zaidi nchini Tanzania ili kukidhi mahitajio muhimu ya watanzania kama kuelimishwa,kuhabarishwa,kupata taarifa sahihi juu masuala mbalimbali nchini mwao na fursa ya kutangaza matangazo yao ya kibiashara hivyo kutanua wigo wao kibiashara ndani yaTanzania na Hata Kimataifa.


Malengo haya ni makubwa sana katika kuhakikisha Tanzania na watu wake inasonga mbele kimaendeleo kwa kuwashinda maadui watatu wa maendeleo yao ambao ni Umaskini,Ujinga na Maradhi.


Kwa utafiti uliowazi maadui hawa bado ni tishio kwa maeneo mengi sana nchini Tanzania hususani Maeneo ya vijijini, elimu rasmi na isio rasmi kwao bado ni kitendawili hii ni kutokana na ukosefu wa watu hasa waandishi wa habari walio tayari kwenda vijijini kuwasikiliza wananchi na kuandaa vipindi mbalimbali kama makala na vinginevyo vyenye kuwasemea watu ili sauti zao ziweze kusikika hivyo kupata suluhu ya kudumu juu ya matatizo yao yanayowakabili.


Kwa kuthibitisha haya Mkurugenzi wa tovuti hii ya Irunde Reports Bwana Irunde katika maelezo yake alieleza kusikitishwa kwa kile alichosema elimu duni inayotolewa na vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania huku akibaini kuwa Tanzania Bado inauhitajio mkubwa sana wa waadishi wa habari wenye kufanya kazi kwa moyo na kuchimbua mambo kwa umakini kuliko kushadadia mambo kama ilivyo kwa sasa.


“Watu ulimwenguni wanafurahia mfumo wa KIDIGITI kama mabadiliko ya sayansi na Teknolojia lakini mwananchi wa Tanzania hadi leo hamfahamu hata Raisi anayemwongoza,unafikiri mwananchi kama huyu anaweza kuendana na mabadiliko kama haya?,hii ni changamoto kwa waadishi wa habari kufanya kazi ya kuelimisha umma wa watanzania nasio kujaza vipindi vya mapenzi na vitu visivyo na tija kwa taifa katika vyombo vyetu vya habari.”alisema Bwana Irunde wakati akifanya mazungumzo na Irunde Reports.


Kidole kimoja hakivunji chawa,kwa kuzingatia usemi huu Mkurugezi wa tovuti hii bwana Fedinand irunde anawaalika watu na mashirika,taasisi za umma na za binafsi,asasi za kiraia na vituo mbalimbali vya haki za binadamu kuungana pamoja na tovuti ya  Irunde Reports. 


kwa kuifanya tovuti hii kuwa nambari moja kwao katika kutimiza mahitajio yao.


Mwaliko huu unaambatana na taarifa rasmi ya kutoka kwa mkurugezi wa tovuti hii kwamba kwa watakaokuwa tayari kushirikiana pamoja na tovuti hii watapata ofa ya kutangaziwa matangazo yao ya aina yeyote kwa punguzo la Bei la hadi 50% hii ni kama dhamana ya uanachama wao na Irunde Reports.


MALENGO


Malengo ya tovuti hii ni kuchochea mabadiliko katika nchi,kuleta u  na uwajibikaji sahihi kwa pande zote,mfano viongozi wenye dhamana serikali wanatakiwa kuwajibika kwa wananchi wao,pia wananchi wanapaswa kuwajibika kwa serikali yao katika shughuli za kuleta maendeleo ndani ya nchi yao.


Hayo ndio malengo makuu ya tovuti hii, malengo haya yamepangwa kutimizwa na tovuti hii kwa mipango ya malengo ya muda mfupi na ya muda mrefu kwa njia zifuatazo.


• Kufanya tafiti mbalimbali za kihabari katika sehemu za vijijini ili kujua uwajibikaji wa wananchi na viongozi wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo.


• Kufanya mkutano wa pamoja na wanakijiji wa kijiji husika pamoja na viongozi wao wakijiji kujadili masuala muhimu ya kijiji chao na changamoto zinazowakabili na kutoa maamuzi juu ya nini kifanyike.


• Kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu serikalini ili kupata suluhu juu ya kile kichojadiliwa na wanakijiji husika katika mkutano wa hadhara.


• Kuandaa vipindi vya redio na runiga hususani makala ambayo yanatokana na kile kilichojadiliwa katika mkutano huo wa hadhara katika kijiji husika.


• Kufanya tathmini ya utekelezaji wa masuala yaliyojadiliwa kuona je utekelezaji wake umekidhi mahitajio ya wanakijiji?

Njia hizo hapo juu ndio dira halisi ya Tovuti hii katika kufanya kazi ya kupaza sauti zitokazo katika Ardhi ya Tanzania.

USICHELEWE WASILIANA NASI Irunde Reports.


Mission


KUZIFANYA SAUTI ZA WATANZANIA ZISIKIKE NA KUTOA SULUHU YA MATATIZO YANAYOWAKABILI.


Post a Comment

  1. Hakika Hayo ndio Majukumu ya Kiuandishi kila Kheri ๐Ÿ™Œ

    ReplyDelete
  2. Irunde Reports Hakika Mmejipanga Kuihabarisha Jamii

    ReplyDelete

 
Top