Jeshi la polisi Kitengo cha Usalama Barabarani limewataka Madereva, Wamiliki na mawakala wa Mabasi mbalimbali nchini kutimiza wajibu wao ili kuondoa ajali barabarani hasa katika kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu.

Akizungumza Mara Wakati Akiongoza Zoezi la ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi Misuna Kamanda wa Usalama barabarani nchini SACP Ramadhani Ng’anzi Amesema Jeshi Hilo Hatawafumbia Macho Madereva Wanaovunja Sheria za Barabarani Kwani Kufanya Hivyo Kutasaidia kuondoa Makosa yanayoweza kusababisha Ajali na Kupoteza Nguvu kazi ya Taifa.

Amesema Maeneo ambayo wamejikita Kuyakagua ni Mwendo kasi, Hali ya ulevi kwa Madereva na Matumizi ya Ving’amuzi Vinavyoratibu Suala la Mwendo Kasi wa Mabasi huku Akibainisha Kuwa lengo ni kuondoa dhana iliyojengeka kwa jamii kuhusu ajali nyingi kutokea kipindi cha mwisho wa Mwaka.

Kamanda wa Usalama barabarani nchini SACP Ramadhani Ng’anzi Akizungumza na Madereva Hawapo Pichani
Mkurugenzi wa Barabara kutoka mamlaka ya udhibiti usafiri wa ardhini LATRA, Johansen Kahatano amesema Mamlaka hiyo imeendelea kuwakumbusha Mawakala kuwatoza abiria wao kiasi halali cha nauli kama kilivyopotishwa na mamlaka hiyo.

Amesema Katika Ukaguzi huo Jumla Mabasi Sita yamezuiliwa Kuendelea na Safari Kutokana na Kutokidhi Vigezo Kulingana na Ukaguzi wao.

Cc @irundetz

#irundereports


Post a Comment

 
Top